MABINGWA wa
Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki jioni
hii.
Huo ulikuwa
mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki
Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.
![]() |
| Wachezaji wa
Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao, Ismail Dunga kulia |
Hadi
mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na
kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya
44.
Refa Charles
Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari
kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid
Aucho.
Yanga
walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za
kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo,
ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na
kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza
Hamisi Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa
nafasi za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na
Oscar Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga
iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar
alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya
leo.
Hii ni mechi
ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi
akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja
ametoa sare.
Yanga SC;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda,
Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker FC;
George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti,
Khalid Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert
Omonuk,


No comments:
Post a Comment