TIMU sita zimeshakata tiketi ya kucheza
hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji
wenye umri chini ya miaka 20 (U20) wa klabu za Ligi Kuu ya
Tanzania.
Hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya
Karume na Chamazi, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim
Bakhresa kupitai maji Uhai itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo
hivyo.
Timu zilizofuzu kutoka kundi A ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa
Sugar ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha
na Ruvu Shooting ya Pwani wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam
pekee.
Katika mechi zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu)
Coastal Union na Mtibwa Sugar zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, wakati Uwanja wa Azam ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting
mabao 2-1.
Nafasi mbili za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B
zinawaniwa na timu za Simba, African Lyon na Polisi Morogoro. Mechi
itakayochezwa leo saa 10 jioni katika Uwanja wa Chamazi kati ya Polisi Morogoro
na Simba ndiyo itakayoamua timu zitakazoungana na Azam kutoka kundi hilo.

No comments:
Post a Comment