Mtibwa Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14
mwaka huu) imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza
katika mechi ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye
umri chini ya miaka 20 (U20) za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Juma Luzio
alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Alifunga mabao hayo dakika za 44,81
na 88.
Hata hivyo, Toto Africans ndiyo walioanza kufunga katika mechi
hiyo ya kundi A. Bao hilo katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said
Salim Bakhresa kupitia maji Uhai lilifungwa dakjika ya 22 na Pastol
Makula.
Nayo Simba imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya
Tanga katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe
dakika ya 19, Mohamed Salum dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya
89.
Michuano hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting
na Kagera Sugar iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa itafanyika
saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi nyingine
za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), African Lyon vs Azam
(jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na Yanga inachezwa leo
Uwanja wa Chamazi.
Kesho (Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano
hiyo itaendelea Jumapili kwenye viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume na Uwanja wa Azam- Chamazi.

No comments:
Post a Comment